The House of Favourite Newspapers

MAPIGANO NA WANANCHI, POLISI 4 WADAIWA KUUAWA, ZITTO AMPA POLE SIRRO

ASKARI wanne wa Jeshi la Polisi akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi Nguruka – Uvinza, Ramadhan Mdimi wameuawa na wananchi kwa silaha za jadi ikiwamo mishale pembezoni mwa mpaka wa kijiji cha Mpeta baada ya kutokea mapigano baina ya skari hao na wananchi.

 

Inadaiwa kuwa, askari hao walifika katika eneo la Ilunde lenye mgogoro wa ardhi kuwaondoa wananchi wanaodaiwa walianzisha makazi na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji bila kufuata sheria na taratibu za ardhi tangu mwaka 2004.

 

Imedaiwa pia kwamba, wananchi hao walichukizwa na kitendo cha Polisi kuwapora mazao huku wakichoma moto baadhi ya nyumba wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika eneo hilo, iliyofanyika Alhamisi.

 

Mgogoro wa ardhi katika eneo hilo umetokana na kubadilishwa matumizi kutoka ardhi ya kawaida ili iwe ranchi ya uwekezaji hivyo raia wanahisi hawatendewi haki ambapo wananchi wamehoji kwa nini igeuzwe kuwa ranchi wakati wanatozwa fedha za michango ya maendeleo ya jamii na wanapiga kura kuwachagua viongozi na kudai kama shida ni mwekezaji, wako tayari walipe gharama ili waachwe waendelee na shughuli zao.

 

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amempa pole Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro kufuatia vifo vya askari hao huku akisema anaendelea kufuatilia ilikufahamu iwapo kuna wananchi waliodhurika kutokana na mapigano hayo.

BREAKING: Ajali mbaya ilivyoua 5 leo Singida

Comments are closed.