The House of Favourite Newspapers

MAREHEMU B.I.G APEWA MTAA NEW YORK


MAMA mzazi wa marehemu Notorious B.I.G ameweka wazi kuwa mji wa New York umeamua kumpa heshima mwanae kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwenye game ya muziki wa Hip Hop pamoja na mtaa aliokuwa anaishi.


Notorious B.I.G ambaye alifariki miaka 22 iliyopita amepewa moja ya mtaa na kuitwa jina lake, Ms. Voletta ameeleza kuwa mtaa huo utaitwa ‘Christopher Wallace Way’ na umezinduliwa rasmi June 10,2019 katika makutano ya barabara ya St James Place na mtaa wa Fulton Brooklyn Marekani.

Notorious B.I.G ambaye jina lake halisi ni Christopher Wallace alizaliwa May 21, 1972 New York Marekani na kufariki March 9, 1997 kwa kupigwa risasi na enzi za uhai wake aliacha ngoma kibao ikiwemo One more chance, Dead Wrong, Juicy, Who shot Ya na nyingine nyingi.

Comments are closed.