The House of Favourite Newspapers

Marekani: Dreamliner Mpya ya ATCL Hiyooo!

NDEGE mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Boeing 787-8 5H-TCJ Dreamliner ipo katika hatua za mwisho nchini Marekani kuja nchini, ambako inaundwa.

Jana Jumapili, Oktoba 13, 2019, ndege hiyo ilifanyiwa majaribio kwenye Uwanja wa Ndege wa Paine Field (PAE) Seattle nchini Marekani.

Ndege hiyo tayari imeshapewa jina la “Rubondo Island”.

Jana, ofisa wa kitengo cha habari cha kampuni ya Boeing, Jennifer Schuld alituma picha za ndege hiyo na kueleza kuwa ipo kwenye majaribio.

“Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania imeanza majaribio ya kuruka leo. Ndege hii 787 inaitwa Rubondo Island,” aliandika ofisa huyo kwenye ujumbe alioutuma kwenye akaunti yake ya Twitter ikiwa sambamba na picha kadhaa za ndege hiyo.

Comments are closed.