The House of Favourite Newspapers

Marekani Ipo Tayari Kufanya Mazungumzo na Iran

0

MAREKANI imesema iko tayari kujadiliana na Iran bila masharti baada uhasama uliozuka baina ya nchi hizo kufuatia mauaji ya jenerali Qasim Soleimani.

 

Katika waraka uliotumwa na marekani kwa Umoja wa Mataifa, Marekani imejitetea kuwa ilimuua jenerali wa Jeshi la Iran, Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda.

 

Iran ilijibu hatua hiyo kwa kushambulia kwa makombora kambi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq japo hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Na wakati huo huo Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani limepiga kura ya kudhibiti uwezo wa Rais Donald Trump kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran wakati shutuma za Wademocrat dhidi ya mashambulizi ya Marekani kwa Iran zikiendelea.

 

Spika wa Baraza hilo, Nancy Pelosi, ametangaza kura hiyo katika taarifa ambayo inasema shambulio la wiki iliyopita la ndege isiyo na rubani ambalo limemuuwa Jenerali Qassem Soleimani ni la uchokozi na limevuka mipaka.

Leave A Reply