The House of Favourite Newspapers

Uamuzi wa Shauri la Meya wa Jiji la Dar, Kutolewa Kesho Kisutu

0

Uamuzi wa shauri la Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wa kuomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itoe amri ya kusitisha mchakato wa kung’olewa kwenye nafasi hiyo hadi maombi yake ya msingi yatakaposikilizwa umeshindikana kutolewa hadi kesho saa tano kutokana na hakimu hajamaliza kuanda uamuzi huo.

 

Akitoa ahirisho hilo Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega ameeleza kuwa uamuzi wa ahirisho hilo unatokana na mda aliokuwa amepanga kuwa mchache wa kuandaa uamuzi huo hivyo akaomba uamuzi huo autoe kesho Januari 10, 2020.

Mwita anayewakilishwa na Wakili, Hekima Mwasipu aliwasilisha maombi hayo dhidi ya Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda, Halmashauri ya Jiji hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kuzuia ombi la kuvuliwa umeya wa jiji la Dar es Salaam.

 

Wakili Mwasipo aliwasilisha maombi hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega wakati maombi hayo yalipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Alidai wamewasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura na yanalenga kuwazuia Mkuu wa Mkoa, Halmashauri na Mwanasheria Mkuu wa serikali kujihusisha katika mchakato wa kumng’oa kwenye nafasi ya Umeya wa jiji hilo.

Waliomba mahakama izuie mchakato huo au hata kama kutakuwa na kikao chenye ajenda hiyo isizungumziwe na Mkuu wa Mkoa pamoja na Halmashauri wazuiliwe kufanya mchakato huo.

 

Katika kesi hiyo jopo la mawakili wa serikali tayari liliwasilisha mapingamizi kupinga maombi ya msingi yaliyopo mahakamani hapo na upande wa utetezi.

 

Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi kesho saa tano mchana kwa ajili ya kutoa uamuzi wa ama kusitisha mchakato huo au la.

Leave A Reply