The House of Favourite Newspapers

Marekani Kuipatia Tanzania Msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 560

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamla Harris ametangaza ushirikiano na Tanzania katika maeneo mbali mbali ya kiuchumi kisiasa na kijamii.

Bi Harris vilevile ameipongeza serikali ya Tanzania katika suala zima la usimamizi wa demokrasia huku akisisitiza ushirikishwaji zaidi wa wanawake katika demokrasia ambapo ametangaza Marekani kutoa kiasi cha dola bilioni moja kusaidia wanawake katika eneo hilo.

Marekani inatarajia kutoa Dola za Kimarekani milioni 560 kama msaada rasmi kwa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2024.

Katika hatua nyingine leo Machi 31, 2023 Wizara ya Biashara na Viwanda ya Tanzania na Wizara ya Biashara ya Marekani zinatarajia kusaini Hati ya Makubaliano (MOU) kuanzisha majadiliano rasmi ya kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Katika mwaka wa fedha 2024, utawala wa rais Biden umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusiana na demokrasia, haki na utawala nchini huku maeneo mengine ya uwekezaji pia yakigusiwa katika ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania.

Leave A Reply