The House of Favourite Newspapers

Marekani Kupunguza Nusu ya Gesi Chafu Ifikapo 2030

0
                                                Rais wa Marekani Joe Biden

RAIS wa Marekani Joe Biden ameahidi kupunguza hadi nusu, kiwango cha gesi chafu kinachozalishwa na nchi yake ifikiapo mwaka 2030. Biden ametoa tamko hili alipokuwa anaufungua mkutano wa kilele wa mazingira duniani.

 

Biden amezishinikiza nchi zingine zinazosababisha kutolewa gesi hizo chafu kwa kiwango cha juu, kupunguza ili kwenda sambamba na makubaliano ya kimataifa.

 

Marekani ni mharibifu mkubwa kabisa wa mazingira kuliko nchi nyengine yoyote duniani lakini lengo hilo lililotolewa na Biden la kupunguza utoaji wa gesi chafu kwa nusu kiwango kinachotolewa na Marekani kwa sasa, ni jambo ambalo huenda likachochea serikali za nchi zingine kufuata hatua za kupunguza gesi hiyo.

 

Kama sehemu ya amri yake ya utendaji aliyoitia saini katika siku zake za kwanza afisini, Biden alitangaza mpango mpya wa mazingira, wa jinsi Marekani itakavyoshirikiana na Benki ya dunia na Shirika la fedha duniani IMF kuzisaidia nchi maskini kupunguza utoaji wa gesi chafu kwa ajili ya kuyalinda mazingira.

 

Leave A Reply