Marekani yaikamata meli ya Korea Kaskazini kwa kukiuka vikwazo

 

MAREKANI imeikamata meli ya Korea Kaskazini ikiilaumu kwa kukiuka vikwazo vya kimataifa. Wizara ya Sheria imesema kuwa meli hiyo ilitumika kusafirisha makaa hayo ambayo ndiyo biashara kubwa ya taifa hilo licha ya kupigwa marufuku na Umoja wa Mataifa kuendelea kuyauza nje

 

Meli hiyo ilikuwa imekamatwa nchini Indonesia mnamo mwezi Aprili 2018.   Ni mara ya kwanza Marekani imeikamata meli ya Korea Kaskazini kwa kukiuka vikwazo na hatua hiyo inajiri wakati ambapo uhusiano kati ya mataifa hayo mawili umedorora.

 

 

Mkutano kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, na Rais wa Marekani, Donald Trump, uliisha bila makubaliano mnamo mwezi Februari mwaka huu huku Marekani ikiisisitizia Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa kinyuklia na Pyongyang nayo ikisisitiza kuondolewa vikwazo dhidi yake.

 

 

Korea Kaskazini imefanya majaribio mawili ya makombora yake angani katika kipindi cha wiki moja katika kile kinachoonekana kuwa jaribio la kuishinikiza Marekani kufanya makubaliano.

Loading...

Toa comment