The House of Favourite Newspapers

Marioo Afunguka Mazito “Mimi na Mondi Tunaliamsha Muda Wowote”

0
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Marioo.

 

MUZIKI ni ajira, lakini pia ni biashara kubwa ndiyo maana nchini Nigeria wanaichukulia serious tofauti na wengi wanavyoiona!

 

Kila mwaka wanazaliwa wasanii wapya ambao wanakuja kuwa wakubwa na kukimbiza ndani na nje ya nchi ndiyo maana huwezi kushangaa kuna kipindi wanaibuka hata watano au saba kwa mpigo na wote wakakubalika.

 

Tumeona kipindi wanaibuka Davido, Yemi Alade, Wizkid, Burna Boy na nwengine ambao leo ni wasanii wakubwa.

Kibongobongo wasanii wengi wamekuwa wakizaliwa, lakini siyo kwa kiwango cha kutoboa kimataifa, lakini wameendelea kudumu kwenye gemu.

 

Kipaji, uchapakazi na kutokata tamaa, ni kati ya mambo yanayomfanya kijana huyu kutokea katika maisha ya chini na kuwa gumzo kwenye gemu ya muziki wa Kizazi Kipya.

 

Anasema alianza kazi hii kwa kuwaandikia wasanii wengi ngoma kali zilizotamba.

“Napambana sana kwenye muziki kwani kabla ya hapa nilishawahi kufanya kazi za kwa mama ntilie mgahawani,” anasema Marioo.

 

Sasa Marioo anafahamika kwa ngoma zake kali kama

 

Dar Kugumu, Manyaku, Ifunanya, Inatosha, Raha, Chibonge alioshirikishwa na Abbah Process, Weka, Mama Amina, Beer Tamu, Mi Amor, Naogopa akiwa na Harmonize, La La na nyingine kibwena.

 

Marioo ambaye jina lake halisi ni Omari Mwanga anasema amezaliwa mwaka 1995 jijini Dar na akiwa bado mdogo, wazazi wake walimpeleka kuishi kwa bibi yake huko Rufiji mkoani Pwani.

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Marioo kuingia kwake kwenye muziki kulitokana na kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na changamoto za kifamilia.

 

Anasema jina Mario (linatamkwa Marioo) limetokana na jina lake halisi ya Omari, akiitoa herufi ya kwanza O na kuipeleka mwisho wa jina.

 

Marioo amejizolea umaarufu baada ya kuwatungia ngoma wasanii wengi wakubwa kama Nampa Papa ya Gigy Money, Pambe wa Christian Bella, Nabembea wa Ditto, Bado ya Mwasiti, Sawa ya Msami na Wasikudanganye ya Nandy.

 

Wachache wanalitambua hilo kwamba hadi wale wakongwe kuna muda wanapungukiwa busara za kuandika mashairi hivyo kuomba msaada ili kuendelea kupeta kimuziki.

 

IJUMAA SHOWBIZ imefanya mahojiano maalum (exclusive) kwa mara nyingine na Marioo ambaye anafunguka mengi;

IJUMAA SHOWBIZ: Mambo vipi Toto Bad?

 

MARIOO: Mambo yako poa kabisa tunamshukuru Mungu kwa kweli yanakwenda pamoja na misukosuko ya hapa na pale.

IJUMAA SHOWBIZ: Misukosuko ipi tena?

 

MARIOO: Mambomambo tu!

IJUMAA SHOWBIZ: Au kauli ya Mheshimiwa Babu Tale bado imekukaa akilini?

MARIOO: Hayo mimi nimeshasahau kabisa.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Kama umesahau hiyo misukosuko unaipata kwenye nini?

MARIOO: Ni mawazo ya kuweza kupeleka muziki wangu mbali na hapa inanifanya niwe na mawazo sana.

IJUMAA SHOWBIZ: Au nikuhusu Mimi Mars kukukana mbele za watu?

 

MARIOO: Kunikana vipi? Yaani mbona sijakuelewa?

IJUMAAA SHOWBIZ: Kusema kwamba wewe na yeye hakuna mapenzi, ninyi ni marafiki ameizing…

MARIOO: Kwani mimi kuna kipindi nilishawahi kusema kwamba mimi na Mimi Mars ni wapenzi jamani? Mbona mnapenda kukuza mambo?

 

IJUMAA SHOWBIZ: Ila nimesikia akiambiwa ataje kati yako na Diamond nani anamkubali, akasema Mi Amor…

MARIOO: Mi Amor ndiyo nani?

 

IJUMAA SHOWBIZ: Hujui au unajizima data? Mi Amor ni wewe, si una ngoma ambayo uliimba kwa hiyo akaona asikutaje moja kwa moja, Simba asije akamnyima kuongelea kwenye swimming yake!

 

MARIOO: (anacheka) sasa miye tangu lini nikaitwa Mi Amor ila sijalisikia hilo kabisa. Pia nashukuru sana kama amesema hivyo na wewe naye unavyosema Simba akisikia atamnyima kuogelea tena. Mimi nimeshasema namuwekea swimming pool nyumbani asijali kuhusu hilo, watoto wazuri hawahitaji mateso.

 

JUMAA SHOWBIZ: Una nini unataka kuwapa mashabiki wako?

MARIOO: Kwanza kabisa nitake kusema tu kwamba huu ni mwaka mzuri sana kwangu. Pia niwashukuru sana mashabiki wangu kwa sapoti yao, hawajawahi kunipinga kwamba eti ngoma mbaya, wao kila siku sifa kwangu na cha kuwaahidi ni kwamba nitawapa kile roho zao zinapenda.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Umesema kwamba ‘my next single from my album it’s gonna be an anthem kama kawaida yangu trust me!’ Labda matarajio ya kutoa album yako ni lini?

MARIOO: Ni lazima uwe na ngoma ya Taifa, nimeamua kufanya mapinduzi ya Bongo Fleva muda siyo mrefu na ikifika karibu nitafanya jambo ili kuweza kutambulisha.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Na vipi kwenye album kutakuwa na wasanii wa nje au ni Bongo pekee?

MARIOO: Lazima wasanii wa nje wahusike.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Itakuwa na ngoma ngapi?

MARIOO: Hayo yote nitayaweka wazi siku ikikaribia kama nilivyosema lazima nitafanya jambo ili kuweza kuelezea album yangu.

IJUMAA SHOWBIZ: Vipi kolabo yako na Diamond imeishia wapi?

 

MARIOO: Mashabiki wakae tayari muda na wakati wowote goma linaachiwa.

IJUMAA SHOWBIZ: Lakini naona kama upande wa pili (WCB) hawakutaki…

 

MARIOO: Mbona hawana shida? Naona wapo kawaida tu, muziki siyo vita hapa ni baishara ili kuweza kupata kitu.

IJUMAA SHOWBIZ: Hapa siyo dalili ya mvua ni mawingu? Maana nakumbuka siku ya birthday ya Sallam SK alisema uimbe tu mwenyewe, kingine Babu Tale anakuchongea kwa Wabunge?

 

MARIOO: Tuachana na hizo stori ila mashabiki wangu wake mkao wa kula ngoma linakuja la Simba na Toto bad.

IJUMAA SHOWBIZ: Lisemwalo lipo kama halipo basi laja…

MARIOO: Acha lifike mimi ndiyo nalisubiri.

IJUMAA SHOWBIZ: Ahsante kwa ushirikiano wako.

MARIOO: Karibu tena.

”NAPOKEA DM 7000 kwa SIKU, NALIPA WATU PESA WANIOGESHE” – ASHA FEROOZ | DSM FLAVOUR…

Leave A Reply