The House of Favourite Newspapers

Masau Bwire Ataja Sababu Kufungwa 7

0

MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Simba, amesema kuwa ni mambo matatu yamesababisha timu hiyo kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho baada ya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Ruvu Shooting 0-7 Simba.


Juzi Simba ilitinga robo fainali ya michuano
hiyo maarufu kama Kombe la FA, huku mabao yakifungwa na Clatous Chama aliyetupia matatu, John Bocco mawili na Michael Mainda alijifunga pamoja na Jimmyson Mwanuke.


Akizungumza na Championi Ijumaa,
Bwire alisema kuwa kufungwa mabao 7 sio tatizo kwa kuwa tayari wameshatolewa na hata Brazil ilishawahi kufungwa lakini kilichowaponza ni wachezaji kukumbwa na
mambo matatu.


“Kwanza ninaweza kusema ni majonzi,
ikumbukwe kwamba tumetoka kwenye majonzi ya kuondokewa na mchezaji wetu muhimu na tumepiga picha kwa pamoja kumuombea hivyo wachezaji walikuwa wanacheza wakiwa kwenye majonzi.


“Pili ninaweza kusema ni dharau, wachezaji
wetu waliwadharau Simba na kuona ni timu ya kawaida haina madhara, ndio maana tulikuwa hatuzuii bali tunashambulia.

 

“Tatu niseme kwamba kuna suala la majira, wakati na ukombozi, kwa waliopita kwenye maandiko wanaweza wakajua lile tukio la Yusuph familia yake ilitaka kumuangamiza lakini akatokea mmoja akasema kwamba tusimuangamize, Yusuph akapelekwa utumwani na mwisho akawa ni mkombozi kile kipindi cha njaa,” alisema Bwire.

Mchezaji ambaye ametangulia mbele za haki hivi karibuni ni beki kiraka, Ally Mtoni ‘Sonso’ aliyekuwa akiichezea Ruvu Shooting.

Leave A Reply