The House of Favourite Newspapers

Majanga: V8 Yateketea Kwa Moto

0

Gari aina ya V8 imeteketea kwa Moto maeneo ya mwenge, karibu na Chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es salaam.

Gari hiyo iliyokuwa kwenye maegesho eneo la Ofisi ilianza kuungua sehemu ya ndani, kwa mujibu wa mashuhuda hakuna madhara ya binadamu yaliyotokea ingawa mali hiyo imeteketea yote kwa moto, huku mmiliki wa Gari hilo akifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu vichache vilivyokuwemo ndani.

Baadhi ya wananchi kwa kushirikiana na mmiliki wa Gari hilo wamefanya Jitihada za kuuzima moto huo, huku wakisubiri Jeshi la Zimamoto na uokoaji kufika eneo la tukio.

Leave A Reply