Masele Aaga Rasmi Bunge la Afrika

MAKAMU wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Stephen Julius Masele,  ameaga rasmi Bunge la Afrika (Pan-African Parliament – PAP) baada ya muda wake kutumikia Bunge la Afrika kufikia kikomo.

 

Katika ujumbe wake wa kuwaaga wabunge, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa bung hilo, Masele ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (2010-2020) amesema mhula wa Bunge la Afrika na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinaenda sanjari hivyo nafasi yake imefikia tamati baada ya muda wake wa ubunge nchini kufikia tamati.

 

“Mhula wa Bunge la Afrika unaenda samba na mhula wa Bunge la Tanzania.  Baada ya kipindi cha ubunge kuisha ambacho kinaenda na uhai wa bunge la Afrika, nafasi yangu ya ubunge wa Afrika pia imefikia tamati.

 

Kukosa nafasi ya kugombea ubunge kunahitimisha rasmi nafasi yangu katika Bunge la Afrika,” amesema.


Toa comment