The House of Favourite Newspapers

Yanga Ilivyopiga Jalamba Leo Kujiwinda na Msimu Mpya Wa Ligi Kuu Bara

0
Wanaume kazini licha ya mvua ya rasharasha kutaka kutibua mambo.

Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi bara huku wachezaji wapya wa kikosi hicho wakishindana kuonesha uwezo kwenye mazoezi hayo.

Zoezi likiendelea kwa staili hii.

Mazoezi hayo yalifanyika Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo Mawasiliano Dar, ambapo licha ya mvua ya rasharasha kutaka kutibua mazoezi hayo lakini baadae mambo yalikaa sawa.

Farid Mussa mbongo aliyekuwa akicheza soka nchini Hispania na sasa kutua Yanga akikokota mpira.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo beki mpya wa kikosi hicho, Bakari Mwamnyeto aliyetokea Coastal  Union ya Tanga amesema anajua ugumu wa kupata namba kwenye kikosi hicho lakini amejiandaa kikazi kuhakikisha anapata namba ya kudumu kikosi cha kwanza.

Mwandishi wa Champini na Spoti Xtra, Wilbert Molandi akizungumza na kocha anayeendelea kusimamia mazoezi wakati akisubiriwa kocha mkuu.

“Najua sasa hivi nipo kwenye timu kubwa yenye changamoto ya namba lakini nitahakikisha najituma zaidi ya nilivyokuwa ili kuwafurahisha mashabiki wa timu yangu.

Kipa Farouk Shikalo akiizungumzia changamoto ya kukosa nafasi kikosi cha kwanza.

Hii ni timu kubwa hivyo dawa ya kuwa namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza inabidi uoneshe uwezo wa hali ya juu na hilo ndilo lengo langu.

Bakari Mwamnyeto akiahidi kazikazi baada ya kutua kikosini hapo.

Naye kipa wa timu hiyo, Farouk Shikalo raia wa Kenya ambaye msimu uliopita alikuwa na changamoto namba katika kikosi cha kwanza amewasifu makipa anaoshirikiana nao, Ramadhani Kabwili na Metacha Mnata ambao walimpa changamoto na kuahidi kufanya vizuri zaidi msimu ujao.

Msemaji wa Yanga, Hassani Bumbuli akizungumza na wanahabari baada ya mazoezi hayo.

“Metacha na Kabwili ni makipa wazuri na msimu uliopita walifanyakazi yao vizuri ndiyo maana kukawa na changamoto ya namba lakini msimu nitahakikisha najituma kadili ya uwezo wangu”. Alisema Shikalo

Msemaji wa timu hiyo Hassan Bumbuli akizungumza baada ya mazoezi hayo amesema kikosi hicho kesho kitakuwa na mechi ya kirafiki kwa ajili ya kukiangalia kikosi chao kipya na timu ambayo ataitaja hapo baadae.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL      

Leave A Reply