Mbasha Aibuka na Kiki ya Mchumba
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili Bongo, Emmanuel Mbasha ameibuka na kiki ya aina yake tofauti na mastaa wengine baada ya kusema atatangaza mchumba wake mtandaoni ambaye anatarajia kumuoa hivi karibuni.
Mbasha aliibuka na kiki kwamba atatangaza mchumba kwenye mtandao wa Instagram lakini hakufanya hivyo jambo ambalo liliwachukiza baadhi ya mashabiki na alipoulizwa kwa nini aliamua kuwadanganya watu alisema kamwe hawezi kutangaza mchumba mitandaoni.
“Siwezi kumtangaza mchumba mitandaoni, suala hilo la mchumba liko kwa mchungaji wangu hivyo kwenye Instagram nilikuwa natafuta kiki tu ya video yangu ya Hallelujah na siyo vinginevyo,” alisema Mbasha.
STORI: MIKITO NUSU NUSU | RISASI JUMAMOSI
=======================