The House of Favourite Newspapers

Siyo Chips Mayai, Piga Msosi Huu Uwe Fiti Uwanjani -2

0

NI Jumamosi nyingine msomaji wangu nakukaribisha katika safu hii ya afya. Wiki iliyopita tuliona vyakula vinavyofaa kuliwa na mwanasoka wakati ligi ikiendelea.

 

Wachezaji wengi wa Kitanzania hudharau katika chakula na hata mpangilio mzima wa kula, wengi hawajali na wanadhani mazoezi pekee uwanjani ndiyo kitu kinach­oweza kuwasaidia.

 

Wanasoka wengi wanaosifika kwa ubishi au ukorofi wanapofika katika chakula, huwa wapole na utekeleza kila wanachoshauriwa na wataalam wa lishe.

 

Kwa kawaida mchezaji akiwa anacheza ligi, anatakiwa kula vyakula vinavyopaswa kuliwa na mchezaji, sasa tuone jinsi ya kuki­tumia chakula hicho.

 

MUDA WA KULA KABLA YA MAZOEZI

Mc h e ­zaji ana­tak iwa k u l a s a a t a t u kabl a y a m a z ­o e z i , h a p a i n a ma a n a k a m a ma z o e z i y a n a a n z a saa 10:00 jio­ni, mchezaji an­apaswa kula saa 7:00 mchana lakini pia wataalam wa lishe wanasema inapaswa kuwa zaidi ya hapo.

Kwamba, mche­zaji inafaa zaidi apate chakula saa tatu na nusu kabla ya kufan­ya mazoezi, hii ina maana muda unao­faa zaidi ni saa 6:30 mchana ili akafanye mazoezi vizuri.

 

CHAKULA KINACHOFAA

Chakula lazima kiwe na wanga wa kutosha lakini kili­chochanganywa na protini kido­go ili kurahisisha mmeng’enyo au uswagwaji wake tumboni.

 

Mchezaji anaweza kula chakula cha wanga kama tambi au wali kiasi na mboga za majani. Hapa anapaswa kuchanganya na kiasi kidogo cha chakula chenye protini ambacho hakina mafuta na samaki wa kuchemsha anapendekezwa zaidi.

Saa moja kabla ya kucheza maz­oezi au muda mfupi kabla ya kupa­sha misuli moto, mchezaji anawe­za kula matunda kama ndizi mbivu mbili au moja ama tufaa (apple) ili kuimarisha kiasi cha sukari mwilini.

Mchezaji anapaswa kunywa maji maalum yenye kiasi cha glucose mwilini ili kulinda kiasi cha sukari mwilini kinachosaidia nguvu kwa mchezaji.

Usikose wiki ijayo kuona ni chakula gani mchezaji anapaswa kula baada ya kutoka mazoezini wakati huu wa ligi.

Leave A Reply