The House of Favourite Newspapers

Zitto Afunguka Kuitwa Kibaraka wa Wazungu Ishu ya Madini, Mwigamba Kuhamia CCM

0
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuber Kabwe amesema kwamba wanachama waliokihama chama hicho walikuwa na mlengo wa kutokuhitaji chama kinachotawala kutokukosolewa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema kwamba hakuna sababu ya mwanachama kuondoka na kukisema chama hicho kwani kimejidhatiti katika misingi yake ya kiuongozi na kwamba hakiwezi kuwa na malengo ya kukitetea chama tawala bali kitaendelea kukosoa kila pale panapostahili.
 
Amesema kwamba mwanachama mwenye mtazamo wa kutokuhitaji kukosoa yanayofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi basi hawezi kuwa mshindi dhidi ya adui yake.
 
“Watu wote ambao wameondoka kwenye chama wameondoka kutokana na kwamba wamepata fursa nyingine, wameondoka tukiwa tumewaruhusu sisi wenyewe na hata kama wameondoka hatujarusha hata mabango yoyote.
Mwigamba ameondoka si kwa ajili ya ugomvi wowote na tumewatakia kila la heri, chama hakiwezi kumomonyoka hata siku moja na Act tutaendelea kuibua viongozi bora hata zaidi ya Humphrey Polepole, hata mimi wapo walionitengeneza hadi nikafikia hapa nilipo. Kuna baadhi ya watu hawakipendi chama hiki hivyo mtusaidie kuelimisha jamii,” alisema Zitto.

Pia katika hatua nyingine ameendelea kuzungumzia mikataba ya Kampuni ya Madini ya Acacia na Serikali ya Tanzania, kwamba serikali inapaswa kushirikisha wadau katika mikataba inayofanya na makampuni ya madini na si kuendelea na migogoro ya kimikataba.

Sisi tuliopigania mikataba hiyo ya madini tulifukuzwa bungeni, unawezaje kuniita mimi ni kibaraka wa wazungu? Wanaosema hayo wao ndiyo vibaraka. Siku zote tumekuwa tukiwaambia kuhusu hiyo mikataba lakini hawakutuelewa, alizungumza Zitto.
VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply