The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Wamtaka Tunda Kuheshimu Ujauzito

Tunda wa pili (kulia) akiwa na baadhi ya mastaa Bongo

Muuza nyago kwenye video za mastaa wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian ambaye amekuwa gumzo baada ya jina lake kuwa katika orodha ya awamu ya pili ya wafanyabiashara, watumiaji na wasafirishaji wa unga iliyotwaja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, anadaiwa kuwa mjamzito na hajisitiri.

Tunda Kushoto akiwa na rafiki yake

Mashabiki wamemtaka staa huyo ajisitiri kwani mavazi yake kwa sasa yanalionesha tumbo lake ambalo limeanza kuwa kubwa.

“Hatukatai kama Tunda ni staa na tunamfatilia sana ila ajisitiri sana bwana kitumbo ndiii”, alimaliza shabiki huyo huku akiomba kutoandikwa jina lake

Picha ya Tunda iliyozua gumzo mtandaoni

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.