The House of Favourite Newspapers

Mashindano Ya Mchezo Wa Drafti Yamalizika, Naibu Meya Tememe Apongeza

0
Inline image 2
Naibu Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tekeme , ambaye pia ni Diwani wa kata ya Temeke, Feysali Salum , akizungumza jambo.
Inline image 3
Baadhi ya Washiriki wakichuana.
Inline image 4
.. Feisali Salum, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa fainali hizo.

MASHINDANO ya mchezo wa Darfti ya Mstahkimi Meya wa jiji la Dar es Salaa Isaya Mwita yamemalizika leo na kufungwa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Feysali Salum ambapo jumla ya washindi wa tatu waliibuka kidedea na kunyinyakulia zawadi kila mmoja.

Mashindano hayo ambayo yalianza Mei 13 na kufunguliwa na Meya Mwita yalikuwa na jumla ya washiriki 64, yalifkia tamati hiyo jana ambapo mshindi wa kwanza Kiraba Ngibombi ambaye pia ni Mweyekiti wa cahama cha mchezo wa Drafti mkoa wa Dar es Salaam alipata pesa tathilisimu sh.200, 000.

Aidha mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Willium Mgata , maarufu kama Bad Face ambaye alijinyakulia kitita cha sh.100,000 na mshindi wa tatu alikuwa ni Hossein Ally aliyapata zawadi ya sh.50,000.

Akikabizi zawadi hizo kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Jiji, Naibu Meya wa Temeke ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM , Feysali pamoja na mambo mengine alimpongeza Meya Mwita kwakuanzisha mashindano hayo na kuahidi kumuunga mkono.

Naibu Feysali alisema kwamba kutokana na umuhimu aliouonyesha mstahiki Meya wa jiji, atashirikiana nae ili kuwa wawalezi wa chama hicho na hivyo kuwawezesha kwenye mchezo huo.

“ Nampongeza Mstahiki Meya wa jiji kwa kuliona hili jambo, pia kutoa heshma kubwa kulifanya ndani ya kata yangu, amefanya jambo zuri sana, sasa kwa umuhimu huo nipo tayari kumuunga mkono, nitashirikiana nae ili kuwa walezi wa chama hichi” alisema Naibu Feysali.

Aliongeza kuwa,” nataka ifikie mahala, muwe mnaenda kushindana hata mikoani, jambo ambalo kwakushirkina na Mstahiki Meya wa jiji Mwita, Mbunge wa jimbo hili Abdala Mtolea, tutawadhamini , muda wowote ambao mtahitaji nyie” alisisitiza.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo ambaye ndie aliibuka mshindi wa kwanza Kiraba, alisema kuwa alichokifanya Mstahiki Meya wa jiji ni kufungua njia ya mchezo huo na hivyo kusisitiza kwamba kufanyika kwa usajili wa chama hicho.

“ Tunampongeza sana Meya wa jiji kwa kuweza kufanikisha jambo hili, limeonyesha msisimko mkubwa, watu wengi wamejitokeza, hii ni heshma kwake, kwenye mengine kutakuwa na hamasa kubwa zaidi kutokana na hili lililofanyika leo” alisema Kiraba.

Mashindano ya mchezo wa Drafti yalidhaminiwa na Mstahiki Meya wa jiji Mwita , ikiwa na lengo la kuhamasisha michezo mingine iweze kufahamika kama ilivyo kwenye mpira wa miguu na michezo mingine.

Leave A Reply