The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Walionusurika Ajali ya Basi Arusha Wapelekwa Marekani

0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiwaaga majeruhi hao Uwanja wa Ndege wa KIA kabla ya kusafirishwa.
Viongozi mbalimbali wakiteremka kwenye ndege baada ya kuwasindikiza watoto hao.
Muonekano wa ndani wa ndege hiyo.
Vitanda vya ndani ya ndege.
Wanafunzi wakipandishwa kwenye ndege hiyo.
Wazazi wa watoto hao watatu wakionyesha hati za kusafiria za kuingia Marekani pamoja na watoto wao na wako tayari kwa safari.
Mmoja wa marubani wa ndege hiyo akiwa na Mbunge Lazaro Nyalandu kwenye Uwanja wa Ndege KIA baada ya kutua KIA jana.
Muonekano wa ndege ya Samaritan’s Purse iliyokuja kuwachukua majeruhi hao.

Ndege kubwa inayoweza kutumika kama ‘AMBULANCE‘ angani na iliyotoka North Carolina, Marekani kuja moja kwa moja Kilimanjaro, Tanzania kuwachukua majeruhi imeondoka asubuhi ya leo Uwanja wa KIA, Kilimanjaro.

Ndege hiyo ya Samaritan’s Purse DC 8 N782SP imewasili Kilimanjaro Tanzania jana Mei 13, 2017 ikiwa na marubani wanne na wahudumu saba tayari kuwabeba majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwa matibabu.

Rubani wa ndege hiyo, amewaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kwamba baada ya kuondoka, watasimama Cape Verde kuweka mafuta kisha kuelekea Marekani moja kwa moja na wanatarajia kuingia kesho.

Ndege hii imetolewa na shirika la SAMARITAN’S PURSE linalosimamiwa na mtoto wa mwinjilisti mkubwa wa Marekani, Franklin Graham, familia yao baada ya kupelekewa habari za kilichotokea kwenye ajali ya Karatu walikubali kuituma ndege hiyo kutoka Marekani kuja kuwachukua majeruhi Tanzania.

Ndege hiyo imeondoka Mei 14, majira ya mchana ikiwa imewabeba watoto hao watatu na mama zao, nesi mmoja na daktari mmoja wa Kitanzania ambao wataendelea kuwahudumia watoto hao ndani ya ndege hiyo yenye uwezo wa kutoa huduma kama ambulance pia.

Ndege hiyo ikishatua North Carolina, SAMARITAN’S PURSE wameandaa ndege nyingine ambayo pia inaweza kufanya kazi kama AMBULANCE na kuwachukua hadi Jimbo la Iowa ambako Hospitali ya Mercy imekubali kuwatibu wagonjwa hao bure kwa muda wote watakaohitaji matibabu.

Leave A Reply