The House of Favourite Newspapers

Mashinji Atambulishwa Rasmi CCM kwa JPM

0

VIONGOZI  waandamizi watano kutoka vyama vya upinzani wametambulishwa leo na kupokelewa rasmi kuwa wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho,  John  Magufuli,  na wajumbe wa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Ofisi Ndogo ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam.

Viongozi hao ni aliyeahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dkt. Vincent Mashinji; aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha kupitia Chadema, Kalisti Lazaro na aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya (Chadema), Mchungaji David Mwashilindi.

Wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Tandahimba (CUF)  Katani Ahmed Katani na aliyekuwa Naibu Meya wa Jiji la Mbeya (Chadema), Fanuel Kyanula.

MAKAMU WA RAIS TFF ALIVYOZINDUA GARI LA WASOMAJI WA CHAMPIONI NA SPOTI XTRA

Leave A Reply