The House of Favourite Newspapers

MASIKINI! Mrembo wa Ini, Figo, Moyo, Kibofu Afariki!

INASIKITISHA sana! Zakia Mohammed (18), mkazi wa Tabata jijini Dar ambaye wiki iliyopita Gazeti hili la Uwazi liliandika habari yake akiomba msaada ili aweze kutibiwa tatizo la figo, moyo, ini na kibofu cha mkojo, amefariki dunia.

 

Mama mzazi wa binti huyo, Fatuma Chakame alisema mara baada ya habari hiyo kutoka, wapo walioanza kujitolea ili kuokoa uhai wa mwanaye lakini wakati akiendelea kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alifariki dunia.
“Ndiyo hivyo Zakia amefariki.

 

Mlipoandika ile habari kuna walioanza kujitolea fedha ili atibiwe lakini ndiyo hivyo kumbe Mungu alikuwa ameshapanga lake. Nawashukuru tu kwa jinsi mlivyokuwa mstari wa mbele kuhakikisha mwanangu anapata matibabu, Mungu awabariki,” alisema mama huyo.

 

Zakia alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo, ini, figo na kibofu cha mkojo ambapo mauti yalimfika wakati akiendelea kutibiwa katika Hospitali ya Muhimbili. Gazeti hili linatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Zakia na Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Inna Lillah Wainna Ilaih Rajiun.

STORI: IMELDA MTEMA, UWAZI

Comments are closed.