The House of Favourite Newspapers

Mastaa wapya Simba wapewa mikataba migumu, Wawekewa mtego

0

IMEFAHAMIKA kuwa wachezaji wapya wote wa kigeni waliosajiliwa katika dirisha dogo la msimu huu wamepewa mikataba migumu ya miezi sita yenye masharti mazito ya kuichezea timu hiyo.

Nyota hao wa kigeni waliosajiliwa katika dirisha dogo ni kiungo mkabaji Babacar Sarr na washambuliaji Freddy Koublane na Pa Omar Jobe ambao tayari wametambulisha na timu hiyo.

Mastaa hao wote tayari wapo nchini wakisubiria ratiba ya kuanza mazoezi ya timu hiyo, chini ya Kocha Mkuu Mualgeria Abdelhak Benchikha aliyekabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara.

Mmoja wa mabosi kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, wachezaji hao kila mmoja amepewa mkataba wa miezi sita ya kumalizia msimu huu na siyo miwili kama ilivyozoeleka.

Bosi huyo alisema kuwa lengo la kuwapa mikataba hiyo, ni kwa ajili ya kuona ubora wa kila mmoja katika ligi na michuano ya kimataifa na kama kocha asiporidhishwa nao, basi wataachana nao.

Alisema kuwa wamechukua maamuzi hayo, kwa kuhofia kutumia gharama kubwa kuvunja mikataba ya wachezaji hao, baada ya kutoridhishwa na viwango vya wachezaji hao.

Aliongeza kuwa yupo makubaliano mazuri waliyokubaliana nayo ambayo yapo katika mikataba yao, ambayo hayawabani kuachana nao baada ya ukomo wa miezi sita waliyokumaliana ya kuachana.

“Ngumu kumpata mchezaji wa kiwango bora ambaye yupo huru kusajili katika dirisha dogo, wachezaji wote bora wana mikataba hadi mwishoni mwa msimu huu.

“Tulichokifanya ni kuwapa mikataba hiyo ya miezi sita wachezaji wote wa kigeni, ambayo kama wakimshawishi kocha na benchi la ufundi, basi tutawapa mikataba mirefu.

“Lakini kwa sasa tumewapa mikataba hiyo mifupi, yenye sharti la kama wakionyesha kiwango bora tutawaongezea mingine ya kuendelea kubakia hapa Simba,” alisema bosi huyo.

Alipotafutwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally simu yake ya mkononi iliita bila mafanikio ya kupokelewa.

STORI NA WILBERT MOLANDI

Leave A Reply