The House of Favourite Newspapers

MATOKEO STARS: JACK PEMBA AKODI BOTI, AKUSANYA KIJIJI KULA BATA UGANDA- VIDEO

IKIWA ni dakika chache baada ya mechi ya Jumamosi ya kufudhu Afcon, kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Timu ya Taifa ya Uganda, mfanyabishara maarufu nchini Uganda ambaye ni raia wa Tanzania, Jack Pemba alikodi boti kisha kuchukua mashabiki wake kwenda kusherekea matokeo ya mchezo huo.
Katika mechi hiyo ambayo Stars chini ya nahodha Mbwana Samatta ilitoka sare ya bila kufungana na Uganda, Pemba alisema kabla ya mechi mashabiki hao walikuwa wakimpa presha kuwa Stars itafungwa lakini haikua hivyo jambo lililompa furaha kuamua kukodi boti ili akale nao bata kujipongeza.

 Aidha, pemba amesema tayari ameshamalizana na TFF ambao walimuomba kwa ajili ya kuja kuwekeza kwenye soka la Tanzania na muda siyo mrefu atarejea kwa ajili ya kuingia mkataba na shirikisho hilo.

MATOKEO Ya Stars, Jack Pemba Ala Bata

Comments are closed.