The House of Favourite Newspapers

Man United Yapigwa, Yatupwa Nje Uefa

MANCHESTER United usiku wa kuamkia leo walishind­wa kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Sevilla, kwenye Dim­ba la Old Trafford.

Huu ulikuwa mchezo wa pili timu hizo zinakutana baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Hispania wiki tatu zilizopita kumalizika kwa suluhu.

 

United ambao hawawezi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, walionyesha kiwango cha chini hali ambayo ilisababisha Sevilla watawale sehemu kubwa ya mchezo.

 

Sevilla walifanikiwa kuwa wa kwanza kupachika bao baada ya mshambuliaji wao mahiri Ben Yedder kuingia kipindi cha pili na dakika ya 74 akaifungia timu yake bao moja baada ya kuwachambua mabeki wa United.

Hata hivyo mshambuliaji huyo alifanikiwa kuifungia timu yake bao la pili katika dakika ya 78 na kuipa uhakika wa kwenda robo fainali.

Romelu Lukaku, ambaye alikosa nafasi nyingi kwenye mchezo huo alifanikiwa kuifungia timu yake bao moja la katika dakika ya 84, lakini halikuweza kuipa timu yake ushindi.

 

United ambao wametwaa ubingwa huu mara tatu, ni uhakika kuwa wanamaliza msimu mwingine sasa bila ubingwa wa Ulaya, ubingwa wa England na labda wanaweza kutwaa Kombe la FA.

 

Kocha wa United alimweka kwenye benchi kiungo wake ghali, Paul Pogba na kumuazisha Marouane Fellaini kwenye eneo la kiungo la timu hiyo ambayo inashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England.

 

Hata hivyo, mwazoni mwa kipindi cha pili Pogba aliingia kuchukua nafasi ya Fellaini, ambapo alionekana hayupo kwenye kiwango kizuri.

 

Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo, Roma walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk na kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya mchezo wa kwanza kuchapwa mabao 2-1 ugenini, hivyo wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini.

Mechi nyingine kali inayosubiriwa leo ni kati ya Chelsea na Barcelona, huku kukiwa na hofu kuwa nao wanaweza kuondolewa.

 

Comments are closed.