Matola: Makocha Ligi Kuu Wanaishi Kwa Presha

KOCHA Msaidizi wa Simba FC, Selemani Matola amefichua kuwa makocha wengi wanaozinoa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, wanaishi kwa presha kwa kuwa hawana uhakika wa kuzipa mafanikio timu zao.

 

Matola amesema hata yeye wakati anainoa timu ya Polisi Tanzania kabla ya kutua Simba, alikuwa anakumbana na hali kama hiyo kwa sababu timu nyingi za chini hazina uhakika wa kushinda michezo miwili mfululizo, huku akiongeza kuwa kwa awamu hii, hali imekuwa ngumu zaidi kutokana na idadi ya timu nyingi zinazoshuka daraja.

 

Matola ambaye aliwahi kuzinoa klabu kadhaa hapa nchini, ikiwemo Lipuli FC, anajulikana kwa sifa ya kuzibana klabu kubwa za Simba na Yanga pindi anapokuwa na kibarua cha kuzinoa timu nyingine.

 

Akizu  ngumza na Championi Jumatano, Matola alisema kuwa makocha wengi wa timu ndogo wanaishi kwa presha kwenye timu zao kwa sababu mara zote wamekuwa wakiishi bila kuwa na uhakika wa kushinda katika kila mechi.

 

Amesema hali hiyo inasababisha waishi bila kuwa na amani kutokana na shinikizo kutoka kwa viongozi wakitaka timu ifanye vizuri, huku akisema msimu huu ni mgumu kwa kuwa kuna timu nyingi zinashuka daraja.

 

“Makocha wengi wanaofundisha timu ndogo wanaishi kwa presha kubwa sana kwa sababu wamekuwa hawana uhakika wa kufanya vizuri katika michezo miwili mfululizo, hivyo mara nyingi wamekuwa wakipata mashinikizo kutoka kwa viongozi na wamiliki wa timu, kwa sababu hata wakati nipo Polisi nilikuwa nakumbana na hali hiyo.

 

“Msimu huu, hali imekuwa ngumu zaidi kwa sababu kuna timu nyingi zinashuka daraja, hivyo kila mtu anapa mbana kuibakisha timu yake,” alisema Matola.

Toa comment