The House of Favourite Newspapers

Matola: Stars Haturudii Makosa

SELEMANI Matola, Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa kilichowakuta mbele ya Sudan kwenye mchezo wa Chan kwa kufungwa bao 1-0 wakiwa nyumbani kimewapa somo, watafanya vema leo mbele ya Equatorial Guinea.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Matola alisema kuwa baada ya mchezo dhidi ya Sudan ambao Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, mashabiki waliwakasirikia makocha na wachezaji.

 

“Hakuna shabiki ambaye alipenda kuona tunapoteza, wengi walikasirika kuona hali hiyo. Imani yao kwetu ilikuwa kubwa na tofauti na awali.

 

“Mashabiki wengi wanahitaji matokeo mazuri hata kama mnaocheza nao ni wagumu, tupo tayari tumefanyia kazi makosa yetu,” amesema.

Comments are closed.