The House of Favourite Newspapers

Matukio 8 Yaliyotikisa Msiba wa Patrick

JUMANNE ya Julai 3, 2018, staa wa filamu kutoka Bongo Movies, Rose Alfonce ‘Muna’ alipata pigo baada ya kufiwa na mtoto wake, Patrick.

Patrick alikuwa miongoni mwa watoto wa mastaa waliotikisa mitandaoni hasa kwa suala zima la ‘kupiga pamba’. Aliugua na kulazwa Agha Khan jijini Dar kisha baadaye kupelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu.

 

Hata hivyo, alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye ubongo ambapo Jumamosi ya wiki iliyopita alipumzishwa katika Makaburi ya Kinondoni.

Nyuma ya msiba huo, yapo matukio mengi yaliotikisa, mvutano ulikuwa mkubwa kujua nani baba halisi wa mtoto, hakukuwa na jibu la moja kwa moja kutokana na mahusiano aliowahi kuwa nayo Muna huku wengine wakidai mtoto alikuwa wa mtangazaji wa runinga, Casto Dickson na wengine wakidai ni wa Peter Zakaria ambaye alikuwa mume wa ndoa wa Muna.

 

Makala haya yanaanika matukio 8 yaliotikisa;

  1. ZAMARADI ACHANGISHA MICHANGO, AJITOA

Kabla na baada ya kifo cha Patrick, mtangazaji huyu wa runinga, alionekana kuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu kutoa michango ya kusaidia matibabu na kuelekeza msiba upo nyumbani kwa Muna (Mbezi Beach).

Ghafla, alibadilisha uamuzi wake baada ya kuona mvutano wa wapi msiba uelekee huku akipewa ‘mbovu’ kwenye mitandao.

 

  1. LULU AONEKANA

Kabla ya kutokea kwa msiba, muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ hakuwa akionekana hadharani, mengi yalisemwa juu yake, mara ana ujauzito mara anataka kuolewa.

Ni mara chache ndiyo alionekana tena kwa siri akiwa sehemu ya kufanyia usafi (Posta jijini Dar) baada ya kutumikia kifungo cha nje kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Baada ya msiba kutokea, Lulu alionekana hadharani akiwa mstari wa mbele kuandaa mazingira nyumbani kwa Muna sambamba na kuwakaribisha wageni jambo lililowashangaza wengi waliofika.

 

 

  1. MUNA AMKATAA MUMEWE

Wakati kukiwa na sintofahamu juu ya baba wa mtoto huku mitandaoni wakimuona Casto ndiye baba wa mtoto, Peter alijitokeza na kusema mtoto ni wake aliyemzaa ndani ya ndoa, Muna hakukaa kimya, naye aliibuka kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram na kuanika kuwa baba mtoto ni Casto.

Hata hivyo, baada ya kusema hayo alifuta posti yake na baada ya muda aliomba radhi na kusema shetani alimpitia na kwamba mtoto ni wa Peter na msiba utakuwa Mwananyamala nyumbani kwake.

 

  1. PETER AMWAGA MBOGA

Katika mahojiano na Global TV, Peter alisema licha ya Muna kuondoka kwake muda mrefu lakini alikuwa akimhudumia mtoto mahitaji mbalimbali ikiwemo suala la ada. Peter alianika cheti cha ndoa, cheti cha mtoto na picha enzi zake za ndoa na nyingie wakiwa na Patrick.

  1. STEVE AINGILIA KATI

Kutokana na mvutano na sintofahamu iliyokuwa imezagaa, mitandaoni wengi walikuwa wakimuulizia muigizaji kutoka Bongo Movie, Steve Nyerere kutokana na uwepo wake na usuluhishi katika misiba mingi hasa ya mastaa wa filamu na Bongo Fleva.

Ilianza kusambaa ‘clip’ ikimuonesha akiwa sebuleni na mume wa Muna, Patrick na kesho yake, aliwahakikishia Watanzania kuwa ameshaongea na Muna pamoja na Peter na kumaliza mgogoro wa wapi msiba uwepo.

 

  1. WEMA AONEKANA TENA

Ikumbukwe kuwa Wema ‘alitrendi’ wiki mbili zilizopita baada ya clip kuzagaa ikimuonesha akiwa mgonjwa ameshikwa na mama yake katika moja ya hospitali jijini Dar. Kabla ya hapo alikuwa kimya mitandaoni.

Mengi yaliongelewa juu yake kutokana na kupungua mwili kwa kasi huku wengine wakiunganisha ‘dots’ kuwa imetokana baada ya kudaiwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo ili kupunguza unene huko India.

Kutokana na ishu hiyo, wengi walitaka kumuona ‘laivu’ alivyopungua na alipotokea kwa mara ya kwanza kwenye msiba wa Patrick, Mwananyamala wengi walimshangaa.

  1. KALALA JUNIOR AIBUKA

Wakati upepo ukianza kutuliatulia, aliibuka msanii wa Muziki wa Dansi, Kalala Junior na kusema kuwa naye ana haki ya kuombeleza msiba kwa kuwa aliishi na Muna miaka mitatu na alimlelea mtoto kama mwanaye.

 

  1. MUNA ASHUKA BILA MWILI

Wakati mwili ukitarajiwa kushuka na Muna Ijumaa iliyopita, hali ya sintofahamu ilitawala baada ya Muna kushuka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akiwa bila mwili.

Licha ya Muna kushuka na kuzimia, bado haikuwekwa wazi mwili ulipo hadi taarifa zilipoanza kusambaa jioni kuwa umekuja bila Muna.

 

BABA PATRICK ACHIMBA MKWARA MZITO KABLA YA KUAGA MWILI – VIDEO

Comments are closed.