MZUNGUKO wa hedhi ni mzunguko wa kila mwezi ambao mwanamke huupata, hali ambayo huleta kutokwa na damu kutokana na mimba kutotungwa.
Kwa hali ya kawaida hedhi ya kwanza hutokea katika umri wa miaka 12 -13 na kuendelea na hutokea pale ambapo tishu za ukuta wa mji wa mimba zinapobomoka na kutoka kama damu ukeni.
Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au ki taalamu dismeno r rhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla y a hapo.
Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation.
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili. Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni
Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Magonjwa pia husababisha mwanamke kusikia maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo.
Leo ninayo orodha ya matunda ambayo yakitumika huweza kupunguza ma umivu wakati wa kipindi hicho.
Matunda hayo ni haya yafuatayo:-
NANASI
Hili ni miongoni kati ya matunda yenye uwezo wa kupunguza maumivu hayo yatokanayo na mzunguko wa hedhi, hii ni kutokana na tunda hili kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa kuifanya misuli ya sehemu za siri za kike kuwa huru (kurelax) na hivyo kupunguza uwezekano wa maumivu makali.
NDIZI
Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa umuhimu wa matunda nadhani utakuwa umewahi kusikia kuhusu umuhimu wa ndizi hata kwa wanamichezo na imekuwa ikiwasaidia kurekebisha misuli na kuondoa tatizo la kukaza kwa misuli mara baada ya mazoezi, hivyo basi tunda hili pia huweza kuwasaidia wanawake ambao wanapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi na kupunguza au kuondoa hali hiyo kabisa.
Pamoja na kukueleza kuwa matunda hayo huweza kupunguza maumivu wakati wa mzunguko lakini ni vyema kuzingatia kuwa matunda hayo yanapaswa kuliwa angalau siku mbili au moja kabla ya kuingia kwenye mzunguko wako ili kupata matokeo mazuri zaidi.
Pia unashauriwa kunywa tangawizi kila siku mara mbili, wiki moja kabla ya kupata mzunguko wako, pia maji ya kutosha kipindi cha mzunguko kwani nayo huwa na nafasi kubwa ya kusaidia kupunguza kiwango cha maumivu hayo.
Papai bichi lililokomaa husaidia kupunguza maumivu ya hedhi unashauriwa kulila mara kwa mara. Mboga za majani pia ni msaada mkubwa kwa kupunguza maumivu.
Comments are closed.