The House of Favourite Newspapers

Mauaji ya Kutisha! Mhadhiri Saut Anyongwa Hadi Kufa Ndani Kwake, Mfanyakazi – Video

0


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT), Hamida Mussa (64) anadaiwa kuuwawa kwa kunyongwa na mtandio shingoni na mfanyakazi wake wa ndani ambaye alitokomea kusikojulikana baada ya tukio hilo kudaiwa kutokea Novemba 29 mwaka huu.

Mwili wa Hamida ulikutwa Novemba 29, 2022 nyumbani kwake mtaa wa Buzuruga mashariki Wilayani Ilemela jijini Mwanza ukiwa umelala sakafuni kifudifudi ukiwa na mtandio shingoni ambapo Mhadhiri huyo alikua idara ya Uhandisi kitivo cha mawasiliano na teknolojia ya habari (ICT) SAUT.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Martin Muya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Mtoto wa marehemu Rehema Mbaga aakisema uchunguzi wa awali uliofanyika kwenye hospitali ya rufaa ya bugando unaonyesha kuwa Mama yake aliuwawa kwa kunyongwa na kitambaa shingoni. ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiC

Leave A Reply