The House of Favourite Newspapers

Maumivu ya Mgongo Tatizo Linalosumbua Wengi

0

MAUMIVU ya mgongo hujitokeza zaidi kwa watu wa umri wa kuanzia miaka 25-40 na kuendelea na ndiyo mara nyingi wanaofika hospitalini kwa ajili ya matibabu. Baadaye nusu ya wagonjwa hupata maumivu makali kuliko ilivyokuwa mwanzoni na ikitokea maumivu yakawa sugu huambatana na matatizo mengine kama vile kukosa usingizi, kusinzia, kulala lakini usingizi huwa mfupi hii ni kutokana na kushtuka mara kwa mara nyakati za usiku.

 

Ukiwa katika umri mkubwa unaweza ukaanza kupata tatizo la maumivu ya mgongo ambayo hukomaa na kuwa sugu. Wengi huumwa mgongo kutokana na kuwa na uzito mkubwa na kutofanya mazoezi, muda mwingi kuketi kwenye kiti kilichosimama nyuzi 90 ukiwa unafanya kazi ya kuandika au kuchapa kazi au kuchora katika kompyuta huku umeinama muda mwingi pengine huku ukichambua majalada lukuki.

 

Lakini pia kusafiri muda mrefu huku muda mwingi ukiwa umeketi kwenye kiti cha gari, ni sababu nyingine ya kuugua mgongo hasa kama mnapita katika barabara zisizo na lami zenye matuta na mashimo.

 

Kuugua mgongo kunasababishwa na kazi tunazofanya, aina za kazi tunazofanya, kusogea kwa umri, kutokuwa na muda wa mazoezi, kuzaa mara kwa mara, zaidi ya yote miili yetu na mienendo yetu kimaisha ikichangia kwa kiasi kikubwa. Maumivu ya mgongo ni moja ya matatizo ya kiafya yanayojitokeza mara kwa mara na huathiri zaidi misuli na mifupa ya mgongo.

Tatizo hili Iinawaathiri karibu asilimia 40 katika moja ya hatua za maisha ya watu Maumivu ya mgongo yapo ya kawaida, yapo ya kati na maumivu sugu ambayo ni zaidi ya wiki 12. Maumivu haya yakiainishwa zaidi yanaweza kutokana na kupata majeraha ya kawaida au mambo yasiyo ya majeraha na chanzo cha maumivu haya kinaweza kuwa eneo husika au maumivu yalitokea mahali pengine mwilini.

 

Mara nyingi maumivu haya chanzo na sababu hasa hakigunduliki moja kwa moja na yakijitokeza mapema, inaaminika kuwa chanzo chake huenda yametokana na kujeruhiwa kwa misuli au mifupa ya mgongo. Pale endapo itatokea maumivu hayo kutoisha baada ya matibabu ya kawaida ama kuambatana na viashiria hatari kama vile kupungua uzito kusikokuwa na sababu maalum, homa kali, kushindwa kuhisi chochote maeneo ya makalio au miguu na kushindwa kujongea vizuri, hali kama hizi lazima hatua za haraka zitahitajika kwa ajili ya uchunguzi kwani ni kawaida maumivu ya mgongo kupotea baada ya matibabu chini ya wiki 6 kwa asilimia 40-90 ya wagonjwa.

KUHUSU MGONGO

 

Umbile la mgongo ni kama vile herufi S likiwa na maeneo makuu matano, kitaalamu huitwa cervical, thoracic, lumber, sacral na coxgeal. Mgongo unaundwa na pingili za vifupa 24 vilivyoshikizwa na kutengeneza maungio, pia kuna vifupa tisa vilivyoshikamana katika mwishilio wake ndiyo unaona kama vile mkia, ndiyo inafanya jumla ya mifupa 33. Katikati ya pingili hizi huwa na sahani kama plastiki, pia huwa na matundu ya pembeni na kati, na kutengeneza mfereji maalum unaopita uti wa mgongo.

 

Uti wa mgongo ndiyo chanzo cha maelfu ya mishipa ya fahamu inayopeleka na kuleta taarifa za mfumo wa fahamu toka sehemu mbalimbali mwilini na kuzipeleka katika ubongo kwa ajili ya tafsiri. Kifupa cha kwanza na cha pili ndivyo vinavyoweza kwenda kujongeza mambo mbalimbali kama vile unaposema ndiyo na hapana kwa mwitiko wa kichwa, vile vile mifupa 12 ya mbavu hukutana na pingili za mifupa ya mgongo na kutengeneza ungio. Kazi kuu ya mgongo ni kuuwezesha mwili kuwa na umbile maalumu linalowezesha mwili kusimama, kuulinda uti wa mgongo ambao ni rahisi kudhurika, ni kiunganishi cha kichwa na kiwiliwili na vilevile mwishilio wa mgongo ndiyo kwa kiasi kikubwa unatusaidia kutembea.

 

DALILI ZA MAUMIVU Mara nyingi mtu huweza kuhisi maumivu pale mtu anapotaka kunyanyua kitu, kunyanyuka na kupiga hatua, kujipinda au kujinyoosha. Itaendelea wiki ijayo…
Simu: +255 753-644 644 / +255 713-112 112

Leave A Reply