The House of Favourite Newspapers

Mauno Yasimamisha Ujenzi wa Barabara

0

DUNIA Uwanja wa Fujo ni riwaya iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi, ikielezea jinsi maisha ya duniani ni sawasawa na fujo! Ndivyo alivyosikika mmoja wa watu walioshuhudia tukio la warembo watatu waliokuwa wakikata mauno barabarani na kusababisha kusimamisha shughuli za ujenzi uliokuwa ukiendelea. 

 

Tukio hilo la aina yake lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ujenzi wa Barabara ya Akachube iliyopo Kijitonyama jijini Dar ambayo ujenzi wake unaendelea. Gazeti hili liliwashuhudia warembo hao wakiwavamia mafundi hao na kuanza kuwakatia nyonga za hatari na kuwafanya washindwe kuendelea na kazi.

 

SABABU NINI HASA?

Warembo hao walijikuta wakisimamisha ujenzi huo wa barabara kwa sababu walidai ni mashabiki wa timu fulani ya mpira wa miguu iliyokuwa ikicheza siku hiyo.

ILIKUWAJE?

Ilikuwa hivi; Warembo hao walikuwa wakipita barabarani wakiwanogesha mashabiki barabarani huku wakiyafuata matawi ya timu zao. Walipofika eneo hilo na kuwakuta mafundi hao ndipo walipoanza kuwatetemeshea uno.

 

Kutokana na hali hiyo, mafundi walijikuta wakipigwa butwaa na kushindwa kuendelea na ujenzi kisha kubaki wakiwakodolea macho warembo hao waliokuwa wakiwapandisha mizuka. Ustadi wa kuzungusha nyonga wa warembo hao ulisababisha baadhi ya mafundi wapagawe na kuzama kwenye pochi kisha kuwatunza.

 

 

Wakati hayo yakiendelea, baadhi ya wapita-njia walionesha kustaajabishwa na warembo hao walioamua kwenda kuwabanjukia mafundi hao wakiwa kazini na kuanza kupiga kelele za ‘weweee’. Kelele hizo zilizidi kuwapandisha midadi warembo na kuanza kucheketua ardhini kwa staili ya chura anayenesanesa.

 

Hata hivyo, warembo hao baada ya kuwafanyia mafundi vimbwanga hivyo, waliendelea na safari yao na kuwaacha baadhi ya mafundi joto likiwa limepanda. “Hatari, lakini salama? Ona mpaka ujenzi wa barabara unasimama kwa ajili yao, kweli hawa wamepinda,” alisikika mmoja wa watu waliokuwa eneo la tukio.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

 

Leave A Reply