The House of Favourite Newspapers

Mayele aache mdomo, bila yanga hatoboi – Shabiki Simba

0

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele aache mdomo kwani timu hiyo ndiyo ilikuwa ikimbeba na si kwamba aliibeba kama amabvyo aliwatolea povu Wananchi hivi karibuni.

Mchome amesema hayo kufuatia kauli za Mayele kuwakejeli mashabiki wa Yanga na Tanzania kwa ujumla, huku timu yake ya Pyramids Fc ikiondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.

“Nilimwambia Mayele kuwa Yanga ni timu kubwa kuliko wewe, sasa timu yake imetolewa na Yanga inazidi kusonga mbele, sasa hivi anajisikia aibu. Mayele anatia huruma sana, namuonea huruma.

“Umewatukana wanyonge wa watu hawanashida na wewe, wamepambana kivyao kwa njia zao wametoboa kwenda robo, wewe ulisema umeifikisha timu yao hapo kwa juhudi zako, kwa nini umeshindwa kuibeba Pyramids kwenda robo? Pyramids imetoka. Inamaana Yanga ndiyo ilikuwa inambeba Mayele.

“Kipindi Mayele yupo Yanga waliipiga TP Mazembe home na away, umetoka umekutana nayo kule, timu ile ile Mazembe, haya funga sasa tukuone? Ngoma ngumu, Yanga ndiyo ilikuwa inakubeba ‘nyang’au’ wewe, bila Yanga wewe hutoboi na nchi pekee unaweza kuvimba ukaimbwa ni Tanzania tu, na ukirudi Simba sikupendi,” amesema Mchome.

Leave A Reply