The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu wa Ethiopia Kufanya ziara ya Kikazi kwa siku 3 nchini Tanzania

0
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwa siku 3 nchini Tanzania, kuanzia Februari 29 hadi Machi 2.

Ziara hiyo inayolenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi imetokana na mwaliko kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Ethiopia yana mizizi ya kihistoria yaliyoanzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Haile Selassie wa Ethiopia.

Leave A Reply