The House of Favourite Newspapers

Mayele Afunguka Magumu Ya CAF Kombe la Shirikisho Afrika

0
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, amesema kuwa, kwenye mechi za kimataifa wamekuwa wakikamiwa sana na wapinzani wao.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, baada ya kucheza mechi tatu za Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa Kundi D, imekusanya pointi nne, ikiwa nafasi ya pili.

Mchezo wake ujao ni dhidi ya Real Bamako ambao unatarajiwa kuchezwa Machi 8, mwaka huu, Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ikumbukwe kwamba, Yanga imetoka kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Real Bamako ugenini, hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele alisema kwenye mechi ambazo wanacheza wamekuwa wakikamiwa ikiwa ni pamoja na yeye.

“Kwenye mechi za kimataifa mabeki wamekuwa wakinikamia ili nisifunge, hilo lipo wazi kutokana na kuwa kwenye kasi na wanajua kwamba ninapenda kufunga kwa ajili ya kuipa ushindi timu yangu.

“Kwa mechi zinazofuata hizo tutajitahidi kusaka ushindi kutokana na ukweli kwamba mechi za nyumbani huwa tunakuwa na mashabiki ambao wanatupa nguvu ya kufanya vizuri.

“Hakuna ambaye amekata tamaa, kwa sasa benchi la ufundi limekuwa likitupa mbinu ambazo tunazitumia, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kila wakati, kazi bado ni kubwa,” alisema Mayele.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply