The House of Favourite Newspapers

Mayele Awania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba wa Afrika

0
Karl Toko-Ekambi

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Fiston Mayele amewekwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba wa Afrika.

 

Mayele amewekwa kupitia jarida la Habari za michezo la foot.afrika akiwa sambamba na nyota kadhaa wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Fiston Mayele

Mchakato wa kumpata mchezaji bora wa mwezi Septemba kwa mujibu wa jarida hilo ni kupitia njia ya kupiga kura katika tovuti ya www.foot.afrika ambapo mchezaji atakayepata kura nyingi ndiye atakayeibuka mshindi.

 

Miongoni mwa nyota walioorodheshwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na

  1. Fiston Mayele (YangaSC na DR Congo)
  2. Seko Fofana (RC Lens na Ivory Coast)
  3. Boulaye Dia (Salernitana na Senegal)
  4. Dango Ouattara (Lorient na Burkina Faso)
  5. Karl Toko-Ekambi (Olympique Lyon na Cameroon)
Boulaye Dia

Vigezo vya nyota hao kuchaguliwa kuwania tuzo hiyo ni kutokana na viwango vyao kuwa bora katika Ligi zao pamoja na mashindano ya kimataifa.

 

 

Leave A Reply