The House of Favourite Newspapers

Mayele Bado Ana Jambo Lake na Simba

0

STRAIKA tegemeo hivi sasa wa Yanga Mkongomani, Fiston Mayele amesema kuwa wanahitaji pointi zote za Ligi Kuu Bara ikiwemo dhidi ya Simba.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu atoke kuwafunga Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Katika mchezo huo, Yanga walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifunga na mshambuliaji huyo akimalizia pasi safi ya Farid Mussa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayele alisema kuwa licha ya kuwafunga Simba katika Ngao ya Jamii lakini bado wanahitaji pointi tatu katika ligi.

Mayele alisema kuwa kikubwa wanazitaka pointi tatu za Simba kwa ajili ya kulinda heshima ya timu yao ya Yanga.

Aliongeza kuwa amejipanga vema kuhakikisha wanapata pointi tatu katika kila mchezo wa ligi kwa kutumia vizuri kila nafasi atakayoipata katika kufunga mabao.

\“Pointi tatu kwetu ni kitu muhimu na cha kwanza, hivyo ili tuzipate hizo ni lazima sisi washambuliaji tutumie vema kila nafasi tutakayoipata ndani ya uwanja.

“Na hili tufanikishe malengo yetu ya ubingwa lazima tupate matokeo mazuri katika kila mchezo tutakaoucheza katika msimu huu.

“Na kati ya mchezo ambao tunauhitaji wa pointi tatu, basi ni dhidi ya Simba ambao tuliwafunga katika mchezo wa Ngao ya Jamii,” alisema Mayele.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply