The House of Favourite Newspapers

Mazishi ya Dawood, kaka wa Meneja Mkuu Global huko Bukene

0

10Wanafamilia, akiwemo baba mzazi (aliyevaa kanzu kushoto) wakiweka mchanga katika kaburi la mpendwa wao.

9Mwili ukipumzishwa kaburini.

8…Likipelekwa makaburini kwa mazishi.

7Jeneza lililobeba mwili likiwekwa vizuri.

6Mwili wa marehemu ukiswaliwa.

5Waombolezaji wakipata chakula.

4Wanafamilia wakiuombea mwili wa marehemu.3Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers walioshiriki katika mazishi hayo, ambao (kutoka kushoto) ni Mhariri Mtendaji wa GPL, Richard Manyota, Mkurugenzi wa GPL, Masha Bukumbi,   Amrani Kaima na Ally ‘Uwazi’ wakiwa msibani hapo.

2Mmoja wa waombolezaji akimfariji Abdallah Mrisho (kushoto).

1Mwili wa marehemu Dawood Mrisho ukiwasili kijijini kwao Bukene,  Mkoa wa Tabora.

WIKI iliyopita Ijumaa, Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd (GPL), Abdallah Mrisho,  alipata pigo baada ya kufiwa na kaka yake, Dawood Mrisho, aliyekuwa anaishi Dar es Salaam.

Marehemu aliyefariki katika Hospitali ya Muhimbili, alisafirishwa hadi nyumbani kwao Bukene, Tabora, ambako siku ya Jumapili alizikwa.   Mtandao wa Global ulikuwepo katika mazishi hayo ambayo yako katika picha zifuatazo:

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA ROHO YA MAREHEMU!

(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)

Leave A Reply