The House of Favourite Newspapers

Mbaroni kwa Kumbaka, Kumlawiti Mama Yake Mzazi – Video

JESHI la polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi mmoja, Mazengo Chilatu,   wa kijiji cha Manchali wilayani Chamwino kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mama yake mzazi baada ya kumvamia chumbani kwake akiwa amelala huku mtuhumiwa mmoja akiuawa na wananchi baada ya kukutwa anambaka mwanafunzi wa miaka minane.

 

Akitoa taarifa za kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Gilles Muroto,  amesema mtuhumiwa aliuawa baada ya wananchi wa eneo la Mailimbili katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kumkamata na kumshambulia baada ya kubaka watu watatu kwa nyakati tofauti.

 

Aidha, katika hatua nyingine,  Muroto amesema matukio ya ukatili yameongezeka kutokana na sababu mbalimbali ukiwemo ulevi wa kupindukia, ushirikina na kukumbatia mila potofu ambapo amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuripoti uhalifu ili kukomesha vitendo hivyo.

Comments are closed.