The House of Favourite Newspapers

Mbaroni kwa kuuza bangi mkesha wa mwenge!

0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi MwombejiKamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji.

SONGEA: Kijana Dickson Komba (22) mkazi wa eneo la Lizaboni mjini hapa, anashikiliwa na polisi baada ya kukutwa akifanya biashara ya kuuza bangi, katika eneo ambalo lilitumika kuulaza Mwenge wa Uhuru, uliokuwa mkoani Ruvuma hivi karibuni.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Yahaya Athumani, alilithibitishia gazeti hili kuwa kijana huyo alikamatwa eneo la Kibulang’oma akiwa na gramu 220 za madawa hayo ya kulevya, akiwauzia watu katika eneo hilo lililokuwa na pilikapilika nyingi.

Kamanda Athumani alisema polisi walifanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo baada ya kupenyezewa taarifa na raia wema waliokuwepo eneo hilo na baada ya kumkamata Komba, muda wa saa 12:50 jioni, walimkuta na bangi hiyo mifukoni mwake.

Alisema baada ya kumkamata na kumfikisha kituo cha Polisi mjini Songea kwa mahojiano na uchunguzi zaidi unafanywa kabla ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

Leave A Reply