The House of Favourite Newspapers

Nyamwela achekelea kunengua Australia

0

SUPERNYAMWELA5Stori: Gladness Mallya

MNENGUAJI nyota wa Bendi ya The African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Hassan Musa ‘Super Nyamwela’ ametoboa jinsi alivyochekelea na kupagawa baada ya kufanya shoo ndani ya Bunge la Australia.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Nyamwela alisema alikuwa na ziara ya wiki tatu nchini humo akiwa na kikundi chake cha Ubuntu, ambapo walipata nafasi ya kuingia katika bunge la nchi hiyo na kutoa shoo ya kitamaduni ambayo iliwafurahisha waheshimiwa hao.

“Yaani nimefurahi sana kuipeperusha bendera ya Tanzania nchini Australia kwani sikutegemea, tumepokelewa vizuri na walifurahia sana shoo yetu ya kitamaduni, yaani tumecheza na kuvaa kitamaduni, ilikuwa ni raha sana,” alisema Nyamwela.

Leave A Reply