The House of Favourite Newspapers

Mbasha: Mimi na mwanangu ni vijana!

DAR ES SALAAM: Staa wa muziki wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha amefunguka kuwa anawashangaa wanaomsema vibaya anapojiachia na mwanaye, Elizabeth Emmanuel ‘Lizy’ na kwamba yeye na mwanaye ni vijana ndiyo maana wanafanya vitu vya ujana.

 

Mbasha alisema kuwa, amekuwa akimuonesha upendo wa hali ya juu mwanaye huyo kwani wanakaribia kulingana kwa kuwa alimzaa mwaka 2004 yeye akiwa bado na umri mdogo.

“Watu wanasema ooh…kwa nini ninakwenda kulala hotelini na mwanangu… kwani walitaka nikalale na nani?

“Walitaka nikalale na vimada? Wengine wanahoji kulala hotelini, kwani walitaka tukalale gesti?

 

“Mimi na mwanangu tunapendana na ndiyo maana ninampa mwanangu malezi bora ya baba,” alisema Mbasha ambaye hivi karibuni alitawala mitandaoni kutokana na pozi alizokuwa akiweka na mwanaye huyo wakiwa sehemu za kula bata.

 

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

Comments are closed.