The House of Favourite Newspapers

Mbele ya JPM, Mwenyekiti CCM Ataka Kuwachapa Bakora Viongozi – Video

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye ameonyeshwa kukerwa kwake na vitendo vya viongozi wazembe ambao wanasubili ziara za Rais John Magufuli ili kufanya mambo kwa kurashia huku wakishindwa kusimamia ipasavyo mikakati ya maendeleo katika maeneo yao.

Akizungumza mbele ya Rais Magufuli wilayani Butiama, Kiboye amesema viongozi wa namna hiyo ambao baadhi yao wapo mkoani Mara wanapaswa kuadhibiwa kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kuwatumikia wananchi.

 

“Mhe. Rais, wananchi wa Mara wananipenda kwa sababu mimi ni msema kweli kama wewe, ninaogopa sheria tu lakini isingekuwa sheria ningewalaza chini nikawachapa bakora viongozi wote ambao ni wazembe, wanachelewesha maendeleo, wanashindwa kutatua kero za wananchi, wanaokula rushwa.

 

“Kazi zingine walipaswa wawe wameshazifanya, kero wameshatatua, lakini wanasubili mpaka Rais aje atatue shida kwenye maeneo yao. Rais ana kazi kubwa ya kutuletea meli, maji, ndege na mengine sio vitu vidogo ambavyo mnaweza kuvimalia, mnamchosha Rais wetu.

 

“Mimi nitawasema tu mbele yako hata kama utakuwa umeondoka hapa Mara, ulisema jana kama kiongozi hafai hutasita kumuondoa, ‘kata mti panda mti’ na hawa kata tu!” alisema kiboye.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.