The House of Favourite Newspapers

Kanye Amwomba Radhi Drake Kumaliza Bifu Kati Yao

Kanye na Drake.

Rapa Kanye West amemwomba radhi mwimbaji mwanzake, Drake,   kupitia mtandao wa Twitter akitaka wamalize bifu ya muda mrefu kati yao.

Wawili hao walikuwa katika mtafaruku wa muda mrefu ambapo Drake alikuwa akimkandia Kanye kupitia wimbo wa “Duppy Freestyle” kupitia kwa Pusha T.   Imeripotiwa pia kwamba miongoni mwa bifu kati ya hao ni pale Kanye alipovujisha siri za kile kinachoitwa “mtoto wa Drake” ambapo Pusha aliutumia dhidi yake kupitia wimbo wa “The Story of Adidon”.

Katika kuomba radhi, Kanye, alimtumia Drake salamu za kumtakia kila la heri katika kumaliza mtafaruku kati yao.

Comments are closed.