The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Apagawa Nakiungo Mpya Simba SC

0

BAADA ya kufanya mazoezi kwa muda mfupi na kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na Simba, kiungo mpya wa timu hiyo raia wa Uganda, Taddeo Lwanga, kimemuibua kocha mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck na kusema kuwa kiungo huyo ni mtu hatari na atakuja kuziba pengo la Gerson Fraga Vieira aliyewekwa pembeni.

Sven alisema kiungo huyo ametimia kila idara hasa katika eneo la ukabaji jambo ambalo litaipa ‘balance’ nzuri timu hiyo kama ambavyo alikuwa akifanya Fraga na akiongeza kuwa Jonas Mkude atakuwa na muda wa kutimiza majukumu yake kwa asilimia 100 kwa kuwa amepata mtu sahihi wa kumsaidia.

Fraga aliumia goti ambalo alifanyiwa upasuaji na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa zaidi ya miezi sita hivyo Simba ikalazimika kumsajili Lwanga ili azibe pengo lake.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Sven alisema: “Nimemtazama Lwanga kwa wakati mfupi aliofanya mazoezi na timu, akili yake ya kukaba na kukaa na mpira ni kubwa sana, mwili wake una nguvu sana, naamini lile pengo la Fraga litakwenda kuzibwa, lakini kitu kizuri zaidi Mkude amepata mtu wa kusaidiana naye kwani alikuwa peke yake kwa kipindi kirefu kidogo.”

Lwanga ni moja kati ya mchezaji wa timu ya Taifa ya Uganda ambaye amewahi kuzichezea timu za Express FC, SCV Kampala, Vipers FC na Tanta, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mwili akiwa kama mchezaji huru

Leave A Reply