The House of Favourite Newspapers

Dkt. Tulia Ambwaga Sugu Mbeya Mjini – Video

0

 

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Tulia Ackson ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

 

Ameshinda kwa jumla ya kura 75, 225 na kuibuka kidedea dhidi ya wagombea wengine watano wa vyama vya upinzani akiwamo mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu “Sugu” ambaye amepata kura 37, 591.

 

Wagombea wengine ni Protas Mgaimbila wa Chaumma aliyepata kura 236, Mwakaje Kaili (NCCR-Mageuzi) kura 206 na Rafael Ngonde (CUF) aliyepata kura 88.

 

Matokeo yametangazwa na Msimamizi Mkuu wa Jimbo la Mbeya Mjini, Amede Ng’wanidako, leo Alhamisi Oktoba 29, 2020 katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Wagombea ubunge Mbeya Mjini kutoka chama cha CHAUMMA, Protas Mgimbila, CUF Rafael Ngonde na CCM Tulia Ackson, wamekesha katika ukumbi wa Benjamin Mkapa kushuhudia zoezi la kuhesabu kura.

 

Nunua magazeti kupitia globalapp.co.tz au Application ya GlobalApp Ujishindie Mkwanja hadi Tsh. 100,000/=

iOS 👉 https://apple.co/38HjiCx
Android 👉 http://bit.ly/38Lluc8
Web: www.globalapp.co.tz

 

Baada ya kununua jaza fomu hii bila kusahau jina lako kamili, kumbukumbuku namba ya manunuzi na namba ya simu uliyotumia kununua. Kwa Tsh 300 tu, utakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kujipatia zawadi ya simu mpya na mkwanja mpaka 100,000 kila wiki. Nunua sasa uzawadiwe!

Kujaza fomu bofya hapa ===> https://bit.ly/3oB6AO7

 

 

Leave A Reply