The House of Favourite Newspapers

Rais Zelensky aghairisha mkutano na Wabunge wa Marekani

0

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, alifuta mkutano na wajumbe wa baraza la seneti la Marekani, Jumanne.

Alitarajiwa kuomba kuendelezwa kwa msaada wa kijeshi huku uvamizi unaendelea wa Russia.

“Zelenskyy, hakuweza kutokea kuna jambo limetokea dakika ya mwisho katika mkutano wetu,” kiongozi wa walio wengi katika baraza la Seneti, Chuck Schumer, alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Schumer amesema Zelenskyy, alialikwa kuzungumza kwa njia ya video katika mkutano wa siri ili wale walio kwenye mkutano waweze kusikia moja kwa moja kutoka kwake ni nini kiko hatarini na kuwasaidia wabunge kuupigia kura mswaada unaojumuisha mabilioni ya dola katika msaada mpya kwa Ukraine.

Mkurugenzi wa ofisi ya utawala na bajeti, Shalanda Young alionya katika barua kwa viongozi wa bunge Jumatatu kwamba ifikapo mwisho wa mwaka, Marekani haitakuwa tena na fedha za kutuma silaha na usaidizi kwa Ukraine.

#EXCLUSIVE: DOGO ANAYETRENDI AKIIMBA MUZIKI, AMPA SALAMU ZUCHU, NANDY, PHINA – ”WAJIPANGE”…

Leave A Reply