The House of Favourite Newspapers

MBOSSO AFANYA ‘SHOPPING’ YA NGUVU SPLASH, MAX PUGU MALL

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Yusuf Kirungi maarufu kwa jina la Mbosso (kulia),  akisaidiwa na mfanyakazi wa Duka la Splash na Max yaliyopo Pugu Mall, Ramadhani Juma, kuchagua nguo mwishoni mwa wiki katika maduka hayo ambapo kuna punguzo la bei la 20% kwa mwezi huu.
…Akiendelea kuchagua nguo.
…Akichagua viatu.
Baadhi ya wafanyakazi wa GSM Pugu Mall wakiwa na Mbosso.

 

 

Mwanamuziki wa kizazi kipy, Yusuf Kirungi maarufu kwa jina la Mboso, amewashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kutwaa tuzo ya video bora ya wimbo wake wa hodari iliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda.

 

Mboso amesema tuzo hiyo imempa nguvu ya kufanya vizuri zaidi baada ya kimya cha muda mrefu na kwamba siku chache zijazo ataachia kitu kipya ambacho kitakuwa cha mshindo mkuu katika anga ya muziki wa Tanzania na kuwapa majibu wanaodhani kwamba ameanza kupotea katika anga ya muziki.

 

Msanii huyo ameeleza hayo wakati akizungumza na mwandishi wetu, alipokutana naye katika duka maarufu la Pugu Mall, alikokwenda kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali yakiwemo mavazi akiwa ameambatana na baadhi ya wapambe wake, huku akiwa miongoni mwa wanufaika wa punguzo la asilimia 20 ya bidhaa kwenye duka hilo.

 

Naye Meneja Uhusiano wa Pugu Mall, Matina Nkurlu akizungumzia hatua ya mwanamuziki huyo kutembelea duka hilo na kufanya manunuzi alisema anashukuru sana msanii huyo kufika katika duka hilo na kufanya manunuzi ya nguo na vitu mbalimbali na kujipatia punguzo la  asilimia 20 huku akiwataka mastaa wengine kufika kwenye duka hilo ili wajipatie ofa hiyo.

Comments are closed.