The House of Favourite Newspapers

Mbowe Afikishwa Mahakamani Kisutu – Video

0


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukiwa na ulinzi mkali leo Ijumaa, Agosti 6, 2021 kwa ajili ya kusikiliza Kesi inayowakabili baada ya zoezi hilo kushindikana jana kutokana na muonekano hafifu wa Video Conference.

 

Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo  leo Ijumaa, Agosti 6, 2021 muda wa 2:12 wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.

 

Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama. Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya. 

 

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.

 

 

 

Leave A Reply