The House of Favourite Newspapers

Taratibu za Kufungua Kesi ya Mbowe Zimekosewa, Kesi Yaahirishwa

0

KESI ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeahirishwa leo Ijumaa, Agosti 6, 2021 hadi Agosti 13, 2021 baada ya upande wa Serikali (DPP) kudai kuwa taratibu za kuifungua kesi hiyo Mahakama yenye mamlaka kuisikiliza kesi hiyo kutokamlika.

Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo  leo Ijumaa, Agosti 6, 2021 muda wa saa 2:12 asubuhi wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.

Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama. Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya. Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.

 

Aidha, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Catherine Ruge pamoja na Suzani Kiwanga na wanachama 11 wamekamatwa na Polisi Nje ya Mahakama ya Kisutu na Wamempeleka katika Kituo cha kati cha polisi (central).

 

Leave A Reply