Mbowe Atoa Machozi Akimzungumzia Mzee Lowassa Nyumbani Kwake – Video
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefika kwenye msiba wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kwa niaba ya chama chake na kutoa salamu na pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kifo cha Lowassa, kilichotokea Februari 10, 2024.
Mbowe amemuelezea Marehemu Lowassa kuwa alikuwa kiongozi shupavu na mwanasiasa wa kuigwa aliyeacha alama katika nchi hii.